SERIKALI imesema inaendelea kuwahamisha wananchi ambao nyumba zao hazikuathirika, lakini zipo pembezoni mwa Mlima Hanang, ili kuwaepesha na madhara zaidi.
Msemaji wa Serikali, Mobhare Matinyi akizungumza muda mfupi uliopita amesema serikali bado inaendelea na jitihada za kuwahamisha wananchi hao na kuwatafutia maeneo mengine, huku juhudi za kurejesha huduma muhimu kama maji, umeme zikiendelea.
Kaya 1,150 zenye watu 5600 zimepoteza makazi yake kwenye mji mdogo wa Katesh, na vitongoji vya karibu vya Jorodom, Ganana, Katesh na Dumbeta pamoja na Vijiji vya Gendabi, Sarijandu, Arukushay na Sebasi, wilayani Hanang, mkoani Manyara.