Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliolima shamba la Serikali wapewa siku saba kujisalimisha

Kilimo Tanzania 1140x640.jpeg Waliolima shamba la Serikali wapewa siku saba kujisalimisha

Mon, 24 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Wilaya ya Hanang Bi Janeth Mayanja ameagiza Wananchi waliolima shamba la Serikali la Basotu bila kulipia fedha ya ukodishaji Halmashauri ya Wilaya ya Hanang pamoja na waliojiongezea maeneo kuhakikisha wanalipia ndani ya siku 7 na endapo watakiuka hatua zitaanza kuchukuliwa.

Aidha amemwagiza Kamanda wa TAKUKURU wa Wilaya ya Hanang Bw Samson Sana kuwahoji wote waliolima bila kulipia kujua mamlaka hiyo wameyapata wapi, ikiwa ni pamoja na kuliagiza Jeshi la Polisi kulinda eneo hilo, kuhakikisha hakuna mwananchi anavuna mazao bila kuonyesha risiti ya kulipia shamba inayoendana na ukubwa halisia wa shamba.

Hata hivyo Bi Janeth Mayanja amewaambia Wananchi waliolima bila kulipia fedha ya ukodishaji wasipolipia mashamba mazao hayo yatataifishwa. •

Chanzo: www.tanzaniaweb.live