Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliokufa ajalini Tanga wazikwa Rombo

Athanas Pic Waliokufa ajalini Tanga wazikwa Rombo

Mon, 6 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamia ya wananchi katika Kitongoji cha Kirungu Mokala, Kata ya Kelamfua Mokala wilayani Rombo wamejitokeza kwenye mazishi ya marehemu Athanas Mrema (59) ambaye amezikwa yeye na mwanaye mmoja na mjukuu wake katika eneo moja, huku wengine wakizikwa katika maeneo tofauti jirani.

Mazishi hayo yamefanyika leo Februari 6, katika kitongoji hicho ambapo miili ya ndugu wengine inatarajiwa kuzikwa kesho Jumanne na keshokutwa Jumatano katika maeneo ya Keryo, Shimbi na Keryo wilayani humo.

Ajali hiyo iliyoua watu 14 wa familia moja kati ya 20 ilitokea Februari 4, katika eneo la Magira Gereza, Kata ya Magira Gereza, wilayani Korogwe, Barabara ya Segera - Buiko mkoani Tanga.

Ndugu hao pamoja na majirani walikuwa wakisindikiza mwili wa ndugu yao, Athanas Mrema(59) aliyefariki dunia Februari Mosi, kutokea jijini Dar es Salaam kuja mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya maziko ndipo walipokutana na ajali hiyo mbaya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live