Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliojiandikisha mara mbili Ukerewe kukamatwa

Waliojiandikisha mara mbili Ukerewe kukamatwa

Tue, 29 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Ukerewe. Msimamizi wa uchaguzi Wilayani Ukerewe, mkoani Mwanza, Innocent Maduhu ameagiza watu wote waliojiandikisha zaidi ya mara moja wakamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Agizo hilo amelitoa leo Jumatatu Oktoba 28 ,2019 wakati anajibu hoja za katibu wa Chadema wilaya ya Ukerewe, Revocatus Makalanga ambaye ametishia kuwafungulia mashtaka baadhi ya waandikishaji.

Makalanga amewatuhumu kula  njama hizo ili wanachama wake wakose sifa za kushiriki uchaguzi huo kwa kuwaandika katika daftari  kwa zaidi ya kituo kimoja cha kupiga kura baadhi ya wanachama wa chama chake ili wakose  sifa za kushiriki uchaguzi huo.

Akijibu hoja hiyo Maduhu,  ameagiza wasimamizi wa uchaguzi  wapeleke orodha ya majina ya watu waliojiandikisha  zaidi ya kituo kimoja ili wachukuliwe hatua za kisheria

“Unajua  Makalanga wanachama wako wamevunja sheria na kama ikithibitika mahakamani adhabu yake ni kifungo cha miezi 12 gerezani, au faini  ya Sh300,000 au adhabu zote mbili kwa pamoja,” alisema Maduhu ambae alikuwa akizungumza kwenye   kikao cha  cha kutoa utaratibu wa kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za serikali za mitaa.

“Nawashukuru viongozi wa Chadema kwa kunipa taarifa hizi, ambazo zitanisaidia kudhibiti wote wenye nia ya kuvuruga uchaguzi huu. Nimetoa hadi Saa 6 usiku wa leo kama nilivyoombwa na Mchungaji wa KKKT, Gerad Samwel, atakayefika ndani ya muda huo na kuomba radhi ya kosa lake  hatakamatwa,” amesema.

Pia Soma

Advertisement

Awali, Katibu wa Chadema wilayani Ukerewe, Revocatus Makalanga, ametaka kujua hatma ya wanachama wake 22 ambao wanaonekana kupoteza sifa za kushiriki uchaguzi huo.

“Ndugu mwenyekiti wa uchaguzi , baada ya kubaini tatizo hilo tulikata rufaa ngazi ya kata  lakini hatukujibiwa hadi Jana, ambapo rufaa zetu  zimetipwa,” amesema.

Akifafanua amesema kama tatizo hilo halitapatiwa ufumbuzi  wanakusudia kuwashitaki mahakamani waliousika kufoji sahini za wanachama wao.

Ametaja maeneo ambayo wanachama wake wameathilika zaidi kuwa ni wa kata za Bwiro,Muriti, Namilembe ,Kakukulu na Igalla

Katibu wa baraza la wazee wa Chadema wilaya hiyo Evalst Bihemo amesema suala hilo limepangwa na wapinzani wao kisiasa kwani limewalenga wanachama wao waliopitishwa na chama kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi huu.

Katibu wa Bavicha Wilaya Chisano Charles alisema hatua ya kuongeza vituo  vya kuhandikisha wapiga kura kinyume na taratibu zimechangia kuwepo kwa matatizo hayo hivyo ametaka suala hilo liangaliwe kwa makini ili kuepuka kuvuluga uchaguzi.

Katibu wa UVCCM Wilaya, Victor Leopod amepinga madai hayo kwamba ni uzushi na uongo kwa sababu kila chama kilikuwa na wakala kwa kila kituo hivyo hapakuwa na fursa ya kalani kufanya kinyume na maelekezo.

Hata hivyo, msimamizi wa uchaguzi wilaya ya ukerewe, Maduhu amesema  kuanzia Oktoba 29 hadi Novemba 4, ndiyo muda wa wagombea kuchukua fomu na kuzirejesha hivyo ametaka watu wenye sifa wajitokeze kuwania nafasi za uongozi.

Ambapo anatekeleza majukumu yake kwa kufuata kanuni na sheria hivyo hata sita kuchukua hatua kwa mdau atakaye kwenda kinyume.

Chanzo: mwananchi.co.tz