Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliojenga vibanda kiholela watakiwa kiviondoa haraka

C8cd8abff760cfb7a45a060c8fd5d53e Waliojenga vibanda kiholela watakiwa kiviondoa haraka

Fri, 13 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imewaagiza wafanyabiashara wote waliojenga vibanda katika maeneo yasiyo rasmi yanayotumiwa na wapita njia pembezoni mwa barabara kuondoa vibanda hivyo haraka.

Aidha, waliojenga vibanda hivyo pembezoni mwa majengo ya ofisi wanatakiwa kuondoa kwa kuwa siyo rasmi kwa ajili ya kufanya biashara.

Afisa Masoko wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, James Yuna, alisema hayo alipokuwa akizungumza na wafanyabiashara waliovamia na kuweka biashara zao katika maaneo ya barabara yanayotumiwa na watembea kwa miguu na kusababisha usalama kuwa mdogo.

Alisema agizo hilo ni pamoja na wale wote walioweka meza zao za biashara pembezoni mwa majengo mbalimbali ya ofisi kwa kuwa wamekuwa wakileta usumbufu kwa watumishi.

Alisema maeneo hayo yanatakiwa kuachwa wazi kwa kuwa hayako rasmi na pia siyo salama kwa kufanya biashara ukizingatia kuwa yanahatarisha maisha yao na bidhaa wanazozipanga.

Alisema wapo wafanyabiashara waliovamia maeneo yasiyo rasmi na kukiuka kanuni, sheria na utaratibu wa halmashauri ya jiji kwa kuamua wenyewe kuweka biashara bila kujali usalama huku wakitambua kuwa kufanya hivyo ni kosa.

"Hivyo halmashauri ya jiji inawataka muache wazi maeneo haya ya barabara na yanayotumika na watembea kwa miguu na hata kwa wale walioweka meza pembezoni mwa majengo ya ofisi; tunataka yawe wazi kwa usalama wenu,"alisema.

Aidha, aliwataka wafanyabiashara hao kutotumia vitambulisho kama sehemu ya kuvunja sheria kwa kufanya biashara maeneo yoyote bila kujali maelekezo yanayotolewa na halmashauri.

Alisema vitambulisho hivyo kuwafanya wawe huru katika baishara zao, hawapaswi kuvitumia kama kinga ya kutokutii sheria na maelekezo yanayowataka kufuatwa kwa kanuni na sheria zilizopo.

Chanzo: habarileo.co.tz