Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliojenga kiholela Mwanza kuvunjiwa majengo

RC Kunenge: Wasioridhia Bomoabomoa Waende Mahakamani Waliojenga kiholela Mwanza kuvunjiwa majengo

Mon, 10 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meya wa Jiji la Mwanza Sima Constantine amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji kumchukulia hatua kali za kisheria Mhandisi wa Jiji aliyetoa vibali kinyume na taratibu za Mipango Miji kwa Wamiliki waliojenga vibanda kiholela na kupelekea kuziba vichochoro katikati ya Jiji la Mwanza.

Hayo yamebainika wakati wa ziara ya Meya aliyoifanya maeneo mbalimbali Jiji hilo, ikiwemo Mtaa wa Deluxe na kukuta ujenzi holela ukiendelea bila kufata taratibu za Mipango Miji.

Sima amesema baadhi ya Wahandisi wa Jiji wamekuwa wakiendelea kuwakwamisha kwa kutoa vibali kwa Wamiliki na kuruhusu ujenzi uanze bila kufuata mpangilio wa Jiji unavyoelekeza kwa Wamiliki kufanya ujenzi rasmi

Amesema Wamiliki wote waliojenga kiholela wapewe notisi na uvunjwaji wa majengo yao ufanyike mara moja huku akisisitiza kuanza kwa operasheni maalumu ya kuondoa vibanda vilivyoziba Barabara katikati ya Jiji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live