Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Walioiba nondo wachukuliwe hatua - Waziri Mkuu

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa 660x400.jpeg Walioiba nondo wachukuliwe hatua - Waziri Mkuu

Mon, 25 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Oktoba 25, 2021 ameliagiza Jeshi la Polisi mkoa wa Lindi kuhakikisha wanakamilisha upelelezi na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wa wizi wa nondo 135 za ujenzi wa wodi daraja la kwanza katika hospitali ya wilaya ya Nachingwea.

Ametoa kauli hiyo akiwa mkoani hapo kwa ziara ya kikazi na kulitaka Jeshi la Polisi kuhakikisha wanawafikisha watuhumiwa hao Mahakamani ili liwe funzo kwa watumishi wengine wa wanaotumia vibaya mali za umma.

Mapema jumapili Oktoba 24, 2021 Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kupitia Mganga Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Dk Charles Mtabho, ilithibitisha kupokea jumla ya nondo 100 kati ya 135 kutoka kwa watuhumiwa haowaliokuwa wamechukua vifaa hivyo kinyume cha taratibu.

" Nikweli Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi, lakini sisi kwa upande wetu tumewataka watuhumiwa ambao ni ofisa idara ya ujenzi, daktari wa Hospitali ya Wilaya na mlizi warejeshe mali zilizoibwa kwa njia ya utatanishi na uchunguzi ukikamilika kama ikibainika hawakuhusika tutawarejeshea mali hizi ila tunachotaka ujenzi uendele usisimame" alisema Dk Mtabho.

Aidha tukio la wizi na kupotea kwa vifaa hivyo lilibainika Agosti mwaka huu ambapo walibaini upotevu wa nondo 135 za ujenzi wa wodi hiyo ya kisasa unaotarajia kugharimu Sh183.89 milioni ambapo hadi sasa zimetumika Sh 61 zilitengwa na halmashauri kutokanana mapato yake ya ndani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live