Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliofukiwa na kifusi wafikisha siku ya tatu ardhini, Waziri Biteko awatuliza wananchi

Fri, 4 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Geita. Waziri wa Madini nchini Tanzania, Dotto Biteko leo Alhamisi Oktoba 3, 2019 ametembelea  eneo la Imalanguzu kata ya Lwamgasa wilayani Geita ambako wachimbaji wawili wa madini wamefukiwa na kifusi tangu juzi, kuwataka wananchi kuwa watulivu wakati uokoaji ukiendelea.

Akizungumza na Wananchi na ndugu wa wachimbaji hao, Biteko amewataka kuendelea kuwa watulivu na kusubiri timu ya uokoaji kuendelea na kazi, ikiwa ni pamoja na kuimarisha kuta za shimo lililotitia.

Wachimbaji hao walifukiwa na kifusi Oktoba Mosi, 2019 saa 12 alfajiri wakati wakihamisha vifaa katika shimo walilokuwa.

Mhandisi wa migodi huo wa ofisi ya madini Geita, Joseph Ng'itu amesema kikosi cha uokoaji cha watu 200 kinaendelea na uokoaji kwa kupokezana.

Amesema hadi leo saa 10 jioni walifika umbali wa mita 44 chini ya ardhi kwa kuhakikisha udongo hautitii na kutoa kifusi hicho.

Amebainisha kuwa waokoaji hao wamesema kuna uwezekano udongo kutofika chini kwa kuwa maji yanayotoka ndani ya shimo kuwa masafi.

Pia Soma

Advertisement
Mkuu wa mkoa wa Geita,  Robert Gabriel amewataka wananchi kuendelea kumuomba Mungu ili wachimbaji hao wanaodhaniwa kuwa umbali wa mita 80 kutoka salama.

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz