Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliofaulu la 7 Dar wote kwenda sekondari

860dfec256aaf644e0afcfb6919ffc55 Waliofaulu la 7 Dar wote kwenda sekondari

Wed, 2 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WANAFUNZI wote 76,372 waliofaulu mtihani wa darasa la saba mwaka huu mkoani Dar es Salaam, watajiunga na kidato cha kwanza mwakani kutokana na mazingira mazuri yanayoandaliwa kwa ajili ya kuwapokea wanafunzi hao.

Akizungumza jana, Mkuu wa mkoa, Abubakar Kunenge alisema mazingira hayo ni pamoja na ujenzi wa vyumba vya madarasa takribani 802 vitavyoigharimu serikali zaidi ya Sh bilioni 16 ili kuwapokea wanafunzi hao.

Mbali na miundombinu ya vyumba vya madarasa, Kunenge alisema pia wametenga zaidi ya Sh bilioni mbili kwa ajili ya maandalizi ya samani zitakazotumiwa na wanafunzi hao ambazo ni vitu na meza 38,296.

Alisema maandalizi kwa wanafunzi hao wakiwemo wavulana 37,338 na wasichana 39,034 sawa na asilimia 93.50 kwa ujumla wao, watajiunga na masomo ifikapo Januari 11, mwakani kutokana na ushirikiano mzuri unafanywa na wakurugenzi wa halmashauri zote za jiji hilo.

“Niwatake wazazi wote kuhakikisha wanaweka mazingira mazuri ya watoto wao kuanza shule ikiwa ni pamoja na kufanya maandalizi ya mahitaji ya mapema ili matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi yatakapotangazwa waweze kuwapeleka shule,” alisema mkuu wa mkoa.

Aidha, aliwakumbusha wakuu wa shule zote 161 zilizopo katika halmashauri zote za Jiji la Dar es Salaam zinazopokea wanafunzi wa kidato cha kwanza kuzingatia Waraka wa Elimu Namba 3 wa Mwaka 2016 kuhusu utekelezaji wa elimu ya msingi bila malipo.

Aliwapongeza maofisa elimu, walimu, wajumbe wa kamati za shule katika manispaa pamoja na wadau mbalimbali kwa juhudi, usimamizi na uboreshaji wa utoaji wa elimu uliochangia wanafunzi hao kufanya vizuri katika mitihani hao.

Alisema kutokana na hatua hiyo, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa inaandaa utaratibu mzuri wa kuwapongeza walimu hao ifikapo Januari 20, mwakani kama sehemu ya kutambua juhudi walizozifanya kupata matokeo hayo.

Chanzo: habarileo.co.tz