Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliofariki wakichimba madini wafikia nane

D4E4F46A 861A 419F AF17 4AE59932540B.jpeg Waliofariki wakichimba madini kinyemela wafikia nane

Sun, 12 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Idadi ya wachimbaji wadogo waliopoteza maisha baada ya shimo waliloingia kujaa maji kufuatia mvua iliyonyesha maeneo ya mlimani imeongezeka na kufikia nane baada ya mwili mwingine kuopolewa.

Wachimbaji hao wanadaiwa kuingia kwenye eneo lenye leseni la utafiti usiku na kuchimba kinyemela na wakiwa ndani ya shimo maji ya mvua yaliingia na kuwazidi nguvu.

Mkuu wa mkoa wa Geita Martin Shigella amewataka wachimbaji wadogo kuheshimu maelekezo yanayotolewa na viongozi na kuacha kuvamia maeneo yasiyo rasmi kwa shughuli za uchimbaji.

Aidha amewataka wamiliki wa leseni za utafiti na zile za uchimbaji kuweka ulinzi kwenye maeneo yao ili kuzuia uvamizi unaoweza kusababisha maafa.

Kamanda wa zimamoto Mkoa wa Geita, Hamis Dawa amesema wachimbaji wadogo maarufu kwa jina la manyani wamekua na tabia ya kuingia kwenye machimbo nyakati za usiku kinyemela.

Amesema ili kukabiliana na maafa kama hayo jeshi hilo limeanza ukaguzi wa kukagua mashimo ya uchimbaji na yale yasiyo na sifa yatafungiwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live