Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliofariki ajali ya Mbeya wafikia 15

16265 Ajali+pic TanzaniaWeb

Sun, 9 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbeya.  Idadi ya watu waliofariki dunia katika ajali iliyohusisha magari matano eneo la Mlima Igawilo jijini Mbeya imefikia 15.

Akizungumza na MCL Digital leo, Septemba 8, 2018 Muuguzi Mkuu wa Hospitali  ya Rufaa Kanda ya Mbeya, Dk Petro Seme, alisema jana walipokea majeruhi 15 wa ajali hiyo lakini wawili walifariki wakati wakiendelea kupatiwa matibabu.

Alisema majeruhi wanne walitibiwa na kuruhisiwa na wengine wanaendelea na matibabu.

“Pia tulipokea maiti 13, lakini majeruhi wawili walifariki dunia hapa hospitali. Majeruhi wengine wawili waliopo hapa wapo ICU (chumba cha uangalizi maalum)  na mmoja hali yake si nzuri.”

“Wengi wameumia zaidi kichwani na kuvunjika miguu na mikono na tunaendelea kuwapatia matibabu,” alisema.

Ajali hiyo ilitokea jana saa 11 jioni ikihusisha magari mawili yaliyokuwa yamebeba mafuta, mengine mawili yalikuwa yamebeba viazi na ndizi pamoja na daladala iliyokuwa imebeba abiria kutoka Igoma kwenda Mbeya mjini.

Soma Zaidi:

Magari matano yagongana Mbeya, watano wahofiwa kufa

 

Chanzo: mwananchi.co.tz