Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliofariki ajali ya Dodoma wafikia saba

Fhgunh1WIAElqwF 780x470 Waliofariki ajali ya Dodoma wafikia saba

Mon, 14 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Idadi ya watu waliopoteza maisha katika ajali iliyohusisha Basi la Arusha Express na Lori katika eneo la Mzakwe Dodoma imefikia saba.

Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu leo alipowatembelea majeruhi wa ajali hiyo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Waziri Ummy amesema kuwa watu tisa kati ya 21 waliopokelewa katika hospitali hiyo wameruhusiwa kutoka hospitalini na 11 wanaendelea na matibabu.

Majeruhi hao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na wanaendelea vyema na matibabu.

Ummy amewashukuru watumishi wa hospitali hiyo kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kutoa huduma za matibabu kwa wagonjwa na majeruhi wa ajali hiyo iliyotokea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live