Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliofariki ajali gari la magazeti wafika 10

Ajali Pic Data Waliofariki ajali gari la magazeti wafika 10

Tue, 14 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Idadi ya watu waliofariki kwenye ajali iliyotokea jana katika eneo la Lungumba Kata ya Mahenge karibu na mlima Kitonga mkoani Iringa imeongezeka na kufikia kumi.

Majeruhi mmoja kati ya watatu waliotokana na ajali hiyo, amefariki wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali Teule ya Ilula.

Ajali hiyo ilihusisha gari ya magazeti aina ya hiace, iliyokuwa ikitoka Dar es Salaam kwenda Mbeya kuacha njia na kugonga mti.

Majerihi wawili waliobaki ambao ni dereva wa pili (alikaa kushoto), Hussein Issa Ally na Monica Philly, raia wa Malawi wamehamishiwa katika Hospitali ya Rifaa ya Mkoa wa Iringa wakiendelea kupatiwa matibabu.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, ACP Allan Bukumbi amethibitisha kifo cha majeruhi wa kumi na kwamba miili yote imehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa.

Advertisement Amesema tayari majina ya miili nane yameshatambuliwa na kuyataja kuwa ni Dickson Richard (dereva), Alpha Nyange, Abdul Ally Lyuu, Olivia Kayombo na Olivia Shimwamwe raia wa Malawi.

Wengine ni Shutamite Kadewelo na Benjamu Kadewelo, wote raia wa Malawi.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, Dk Iddy Omary amesema majeruhi wawili waliolazwa kwenye hospitali hiyo wanaendelea vizuri na matibabu

Chanzo: www.tanzaniaweb.live