Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliofariki Kivuko cha Mv Nyerere waongezeka

19376 Pic+vifo TanzaniaWeb

Thu, 27 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Ukara. Idadi ya waliokufa katika ajali ya kivuko cha Mv Nyerere kilichopinduka Septemba 20, 2018 imefikia watu 228 baada ya mwili mwingine kuopolewa leo.

Watu 41 walinusurika katika ajali hiyo.

Mwili huo umeopolewa ndani ya kivuko na wazamiaji na wataalam wa uokoaji wanaoendelea na kazi ya kunyanyua na kukigeuza kivuko hicho.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa ya Mv Nyerere, Isaac Kamwelwe amesema kuna uwezekano wa miili zaidi kuopolewa baada ya kivuko kunyanyuliwa na kugeuzwa.

Soma zaidi: VIDEO: Mitambo, vifaa vya kunyanyua Mv Nyerere vyawasiri Ukara

Chanzo: mwananchi.co.tz