Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Walinzi 3 wauawa wakiwa lindo

CRIME SCENE.png Walinzi 3 wauawa wakiwa lindo

Fri, 23 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Walinzi watatu wa kampuni binafsi ya ulinzi wameuawa kwa kupigwa na ubao kichwani, wakati wakiwa lindo katika eneo la Mtaa wa Shilabela mjini Geita.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP), Ally Kitumbu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza mauaji hayo yalitokea usiku wa kuamkia leo Desemba 22, 2022.

Amesema mpaka sasa majina ya marehemu wote hayajafahamika na uchunguzi wa awali umebaini walinzi hao walivamiwa wakiwa wamelala na kushambuiliwa kwa ubao mzito na mtu asiyejulikana.

Mkuu wa Wilaya ya Geita, Wilson Shimo amelaani vikali tukio hilo na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano kuimarisha ulinzi na usalama ndani ya wilaya kuelekea kipindi hiki cha mwisho wa mwaka.

Wakizungumuzia tukio hilo, wakazi wa mtaa wa Shilabela wameeleza kushtushwa na kusikitishwa na mauaji hayo na kuliomba Jeshi la Polisi kufanya ufuatiliaji, ili mtuhumiwa aweze kutiwa mbaroni.

Joseph Shija ambaye ni mlinzi binafsi ameeleza mauaji ya walinzi mjini Geita yamekuwepo sana na kilichotokea jana ni matokeo ya kukosekana kwa mwarobaini wa kudumuĀ  wa kumaliza tatizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live