Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Walinisema napenda mapenzi, wananitukana matusi" - RC Mbeya mbele ya JPM (+video)

Screen Shot 2020 07 16 At 4.20.11 AM 660x400.png RC Chalamila

Thu, 16 Jul 2020 Chanzo: millardayo.com

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila leo July 16, 2020 akiongea mbele ya Rais Magufuli ametoa sababu kwa nini? aliahirisha kwenda kugombea Ubunge Iringa Mjini.

“Kilichonifanya nibadilishilie gia angani na kuacha kugombea Ubunge ni kwakuwa JPM umefanya makubwa Mbeya, miradi mingi na natakiwa kuisimamia, usichoke kutulea maana Vijana tuna mihemko, namshukuru Mama Mariam RAS Mbeya amenisaidia kunipunguza mihemko” RC Mbeya mbele ya JPM Ikulu ya Chamwino leo

“Nilipofika Mbeya kuna Watu waliendelea kunitukana ona huyu Kijana anajidai na urefu wake, wakati wakijua mimi mfupi, wengine wakasema ona huyu amekuwa muhuni anayependa mapenzi, ndio maana nilioa ili niyatumikie vizuri hayo mapenzi wanayosema nayapenda” RC Mbeya

“Rais nakupongeza sana na nakuomba usichoke kutulea sisi vijana, kuna propaganda nyingi kwenye majiji tunayoyaongoza. Nikiondoka nikaacha miradi yote nikaenda kugombea sijui kama nitakuwa nimetii mamlaka” Albert Chalamila

BREAKING: RAIS MAGUFULI “SIJAMTUMA MTU KUGOMBEA UBUNGE”

Chanzo: millardayo.com