Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Walimu wasimamishwa kazi kwa kuwafanyisha kazi wanafunzi

Viboko Shule Walimu Walimu wasimamishwa kazi kwa kuwafanyisha kazi wanafunzi

Mon, 23 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Walimu wa Shule ya Msingi Mayamaya Jijini Dodoma, Mallika Billa na mwenzake Mohamed Mochiwa wamesimamishwa kazi kwa tuhuma za kuwatumikisha wanafunzi kwa kuwachomesha Mkaa ambapo ni kinyume na utaratibu.

Maamuzi hayo yamechukuliwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Zaina Mlawa dhidi ya walimu hao.

Hatua hiyo imekuja kufuatia mwanafunzi mmoja kujeruhiwa kwa moto wakati akiwa katika kazi hiyo ambapo tuhuma nyingine ni kubebeshwa Magogo, kulima mashamba ya walimu kama vibarua bila ujira na kutowapa wanafunzi taarifa ya mapato ya Mazao ikiwemo Miradi ya Asali

Oktoba 20, 2023, wazazi na walezi walileta vurugu katika shule hiyo baada ya mwanafunzi wa Darasa la 6 mwenye miaka 13 kuripotiwa kuunguzwa na moto wakati yeye na wenzake walipotumwa na walimu hao kuzima moto bila usimamizi tena kwenye muda usio wa masomo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live