Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Walimu wamchangishia fedha za Unifomu mwanafunzi

Walimu Wamchangishia Fedha Za Unifomu Mwanafunzi Walimu wamchangishia fedha za Unifomu mwanafunzi

Tue, 31 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Walimu wa shule ya Sekondari Uwanjani iliyopo Halmshauri ya Mji Tunduma Mkoani Songwe wamemchangia fedha kiasi Cha Tsh 300,000 (laki tatu) Mwanafunzi ambaye Jina lake limehifadhiwa kwaajili ya kununua Sare za shule na madaftari.

Walimu hao Wakiongozwa na Mwl Fakii Lulandala mkuu wa wilaya ya Momba wamefikia uamuzi huo jumatatu Tarehe 29/01/2023 katika ziara ya mkuu wa wilaya ya kukagua wanafunzi walioripoti kuanza kidato Cha kwanza katika shule za Tunduma wilayani humo.

Baada ya kuona Mwanafunzi huyo anapenda kuendelea na masomo na mama yake alimwambia kuwa anaumwa atakapopona binti huyo angeendelea na masomo walimu wameamua kumuomba mkuu wa wilaya aongoze zoezi la harambee ya kumchangia Mwanafunzi huo ili afanane na wenzake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live