Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Walimu, Wanafunzi watumia choo kimoja Sengerema

Sengerema Walimu, Wanafunzi watumia choo kimoja Sengerema

Sun, 28 Nov 2021 Chanzo: mwananchidigital

Shule za msingi nne katika Wilaya ya Sengerema zina upungufu wa vyoo hivyo kulazimika wanafunzi kutumia choo kimoja na walimu.

Shule hizo ni pamoja na Kizugwangoma, Sengerema, Nyampulukano na Mweli ni zenye upungufu wa matundu ya vyoo 60 hali inayopelekea walimu na wanafunzi kutumia choo kimoja.

Shule hizo zinazokadiwa kuwa na zaidi ya wanafunzi 4500 zimekumbwa na kadhia hiyo ya upungufu wa matundu ya vyoo hivyo kuleta adha ya walimu na wanafunzi kupanga foleni kwenye choo kimoja Ili kupishana kupata huduma ya kujistiri.

Diwani wa Kata ya Mishine, Mbugai Majumba ametembelea shule ya msingi Kizugwangoma leo Jumapili Novemba 28, 2021 na kubaini shule hiyo kuwa na upungufu wa matundu ya vyoo 15.

Shule ya Msingi Kizugwangoma yenye wanafunzi wanafunzi 1252 na walimu 28 ina matiundu ya vyoo 8

Kutoka na kukabilia na hali hiyo wadau mbalimbali wamejitokeza kutoa msaada wa vifaa mbalimbali ili kusadia shule hizo lengo ni kuondoa foleni za walimu na wanafunzi kutumia choo kimoja.

Miongoni wa wadau hao nishirika la Viwango nchi TBS limetoa mifuko 80 ya saruji kwa shule zenye upungufu wa matundu ya vyoo ili ziweze kujenga vyoo na kuondokana na kadhia hiyo.

Meneja Kanda ya Ziwa wa Shirikali la Viwango Tanzania (TBS) Joseph Mwaipaja amesema wao kama wadau wa elimu nijukumu lako kama Shirika kusaidia maeneo ambayo yanahitaji Ili kuondoa changamo zilizopo.

"Tunaiomba Halmashauri msaada huu ujikite kusaidia maeneo yaliyoelekezwa ili changamoto hiyo iweze kumalizika" amesema Mwaipaja.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Sengerema, Samson Ndaro ameshukuru Shirika la Viwango Tanzania TBS kutoa msaada huu ambao utasaidia shule hizo kukabiliana na upungufu wa matundu ya vyoo.

"Tuwahakikishe msaada huu utakwenda sehemu ulioelezwa na siyo maeneo mengine" amesema Ndaro.

Chanzo: mwananchidigital