Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Walichokisema CCM, Chadema ajali ya ndege Bukoba

Operanews1667739286057 Bukoba Walichokisema CCM, Chadema ajali ya ndege Bukoba

Mon, 7 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vyama vya siasa- Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) vimetuma salamu za rambirambi kufuatia vifo vya watu 19 na manusura vilivyosababishwa na ajali ya Ndege ya Shirika la Precision Air iliyotumbukia Ziwa Victoria, Bukoba, mkoani Kagera.

Ndege hiyo iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kwenda Bukoba ikiwa na watu 43 ilitumbukia ziwani mita chache kabla ya kutua Uwanja wa Ndege wa Bukoba.

Vyama hivyo vikubwa na vyenye wanachama wengine nchini Tanzania, kwa nyakati tofauti vimetoa taarifa zikielezea kuguswa na ajali hiyo.

Taarifa ya CCM iliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka ilisema chama hicho kinatoa pole kwa Watanzania waliofikwa na msiba.

"Chama kinatoa pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Shirika la Ndege la Precision, ndugu, jamaa na Watanzania wote waliofikwa na msiba huu wa kuondokewa na wapendwa wetu 19, Mwenyezi Mungu azilaze roho zao mahali pema peponi, Amin," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Pia, CCM kimewaombea majeruhi wote wa ajali hiyo kupona haraka huku kikiwataka Watanzania kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na masikitiko.

"Vyombo vyetu vinavyohusika vitaendelea na hatua za uokoaji na uchunguzi wa ajali hii,” alisema Shaka

Katika taarifa ya Chedema iliyotolewa na John Mrema, Mkurugenzi wa mawasiliano na itifaki wa mambo ya nje inaeleza ajali hiyo inaonyesha Tanzania haina uwezo wa kakabiliana na majanga yanapotokea kwa wakati.

"Laiti kama tungekuwa tumejiandaa madhara ya ajali hiyo yasingekuwa makubwa kama ambavyo tumeshuhudia.”

"Tunawapongeza wananchi hasa wavuvi ambao waliwahi mapema eneo la ajali na kutoa huduma ya kuokoa abiria pamoja na ukweli kuwa hawakuwa na vifaa," alisema Mrema

Katika taarifa hiyo ya Chadema imeelezwa kwa hatua ya sasa, wanashauri mamlaka kwenye maeneo yaliyo na viwanja vya ndege watoe elimu juu ya uokozi kwa wananchi walioko jirani na viwanja ili wawe na utayari wa kutoa huduma ya kwanza pindi maafa yanapojitokeza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live