Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Walia wauguzi kuwachotesha ndoo za maji baada ya kujifungua

Ndoo Maji Maji Walia wauguzi kuwachotesha ndoo za maji baada ya kujifungua

Tue, 25 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WANAWAKE katika Halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi wamelalamikia kitendo kinachofanywa na baadhi ya wauguzi hususani katika zahanati za serikali kuwachotesha ndoo za maji mara baada ya kujifungua.

Malalamiko hayo wameyatoa mbele ya Mbunge wa Jimbo la Nsimbo, Anna Lupembe wakati wa ziara yake ya kikazi katika kata ya Uruwila ambapo wameeleza kuwa wanapopata uchungu na kwenda kujifungua katika zahanati za serikali wanapomaliza kujifungua kabla ya kuruhusiwa wamekuwa wakichoteshwa ndoo tano za maji.

Wamesema wanapotakiwa kuchota maji hayo hupitia changamoto kwa kuwa wakati huo ni wazazi na hawana nguvu za kufanya hivyo.

Baada ya kupokea kero hiyo, Mbunge Anna Lupembe ametoa onyo kwa wauguzi wa afya wanaojihusisha na vitendo hivyo kwani vipo kinyume na maadili ya kazi na kuwataka kuzingatia maadili hayo wanapotoa huduma kwa wananchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live