Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Wale wanaokaa na watu ambao siyo raia wa Tanzania wajisalimishe" RC Chalamila

86212 Pic+chalamila "Wale wanaokaa na watu ambao siyo raia wa Tanzania wajisalimishe" RC Chalamila

Thu, 12 Nov 2020 Chanzo: millardayo.com

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, ametoa siku 14 kwa watu wote walioajiri au kuishi na watu ambao siyo raia wa Tanzania, kujisalimisha kwenye mamlaka husika kabla Serikali haijawachukulia hatua kali, akidai kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na wanahatarisha usalama wa nchi.

RC Chalamila, ametoa agizo hilo wakati akizungumza na wafanyakazi wa Shirika la Ugavi wa Umeme nchini, TANESCO tawi la Mbeya na kusisitiza kuwa wale watakaokaidi kutekeleza agizo hilo, baada ya siku 14 kumalizika watakiona.

“Wale watu wote waliokaa na watu ambao siyo raia wa Tanzania wajisalimishe kwenye mamlaka husika, kuna watu wanaishi na wafanyakazi wa ndani kutoka Malawi, kuna watu ni wahudumu wa hoteli siyo Watanzania” RC Chalamila

Katika mkutano wake na wafanyakazi wa TANESCO, RC Chalamila, ametoa maagizo mengine matatu, ikiwemo kuwataka TANESCO kuondoa malalamiko ya wananchi kuhusu kero ya umeme mdogo na wahusika wakaahidi kutekeleza.

LAANA YA KIFO INAYOMUANDAMANA JOE BIDEN, ATAKUFA?, MARAIS 7 IMEWAKUMBA WAKAFA

Chanzo: millardayo.com