Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Walalamikia taka kutozolewa kwa wakati

9f67c8884efbe438a9365af7202dad17 Walalamikia taka kutozolewa kwa wakati

Mon, 22 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WAFANYABISHARA Soko kuu Manispaa ya Shinyanga wamelalamikia kutoondolewa kwa wakati taka zilizowekwa kwenye vizimba vya taka ngumu.

Wafanyabishara walitoa malalamiko hayo juzi mbele ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais(Mazingira) Mwita Waitara baada ya kufika katika soko hilo na kuangalia mfumo wa usafi.

Mwenyekiti wa soko hilo, Alex Stephen alisema taka haziondolewi kwa wakati licha ya kwamba wanachangia kila mmoja kwa mwezi Sh 1,500.

Mmoja wa wafanyabishara sokoni hapo, Athumani Maziku alisema taka ngumu zimekuwa ni kero kipindi hiki cha masika, mvua zinanyesha na harufu ndiyo inaongezeka.

Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Geofrey Mwangulumbi alisema taka zinaingiliana na taka za watu wanaoishi karibu na soko hilo na si wote ambao wanachangia hiyo fedha, ndiyo maana wakati mwingine uzoaji unachelewa kutokana na kijiko cha kuzolea kinakuwa kwenye matengenezo.

Naibu Waziri Waitara aliwataka wafanyabiashara hao watulie kwani serikali inashughulikia malalamiko yao huku akiwataka wafanyabiashara hao kuacha kutumia mifuko ya plastiki inayosababisha kuongezeka kwa taka.

Naibu waziri huyo pia alikagua dampo kubwa la kisasa linalojengwa katika maeneo ya Nhelegani Manispaa ya Shinyanga ambalo linagharimu Sh milioni 200.

Chanzo: habarileo.co.tz