Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Walalamikia rundo la wototo wadogo soko la mitumba

Lango Mitmba.jpeg Walalamikia rundo la wototo wadogo soko la mitumba

Tue, 19 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wafanyabiashara katika soko la kuuza mitumba la Mlango mmoja Jijini Mwanza wamelalamikia baadhi ya kinamama ambao pia ni Wafanyabiashara katika soko hilo kuambatana na watoto wao wadogo na kuwaacha wakirandaranda nyakati za kazi suala ambalo ni hatari kwa usalama wa watoto hao.

Soko hili la Mlango mmoja ni miongoni mwa maeneo ya biashara jijini Mwanza yenye mkusanyiko mkubwa wa watu ambapo wafanyabishara zaidi ya 1000 hufanya kazi zao hapa, lakini hofu ya wafanyabiashara hawa ni watoto wanaokadiriwa kuwa na umri kati ya miaka miwili hadi mitano ambao wamekuwa wakirandaranda sokoni hapa wakati wa kazi jambo ambalo sio salama kwao.

Kwa upande wao baadhi ya kinamama wanaeleza sababu za kuja na watoto wao katika maeneo hayo ya soko, akiwemo mama huyu ambaye hakutaka jina lake litajwe ambaye anasema miongoni mwa sababu ni wanaume kuwaachia wanawake suala la malezi ya mtoto.

'Kinababa warding kwenye majukumu yao wamwogope mwenyezi Mungu watoto wanapata shida humu. Inamaana kule nyumbani tunashindwa kuwaacha kwa sababu ya usalama.'

Naye mwenyekiti wa soko hilo Jackson Antony amesema wameshatoa elimu kwa wazazi hao kutokuja na watoto lakini kutokana na changamoto hiyo kuendelea wanaiomba serikali iwasaidie ili kutafuta ufumbuzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live