Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Walaji kitimoto Dar watolewa hofu

E5f52ded8677208b5a1557a1ce93013c.jpeg Walaji kitimoto Dar watolewa hofu

Sun, 20 Jun 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SERIKALI imewatoa hofu walaji wa nyama ya ngurume maarufu “kitimoto’ katika jiji la Dar es Salaam kuwa hakuna uwepo wa ugonjwa wa ngurume katika jiji hilo.

Hayo yamebainishwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi baada ya kufanya uchunguzi Juni 6, mwaka huu katika maeneo mbalimbali ya jijini la Dar es Salaam kufuatia hofu iliyozuka baada ya nguruwe 298 kufa katika mashamba mawili kwa kile kilichodhaniwa ni ugonjwa wa homa ya nguruwe.

“Baada ya kuchunguza kwa kina kwa wanyama waliokuwa wamebaki kwenye mashamba hayo, pamoja na kuchukua sampuli na kuzipima katika maabara, ilibainika kuwa, hawakufa kwa ugonjwa wa homa ya nguruwe,” alisema Waziri wa Mifugo Mashimba Ndaki

Alisema ufuatiliaji zaidi umefanyika katika maeneo yote ya machinjio ya nguruwe na kuchunguza nguruwe wanaochinjwa na hapakuwa na viashiria vyovyote vya ugonjwa wa homa hiyo ya nguruwe.

Ndaki alisema kuwa wizara yake kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wataendelea na juhudi za kudhibiti kabisa ugonjwa huo nchini.

Chanzo: www.habarileo.co.tz