Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakwe wakumbukwa fao la majanga

Screenshot 2021 08 25 At 19.45.22 660x400.png Mkuu wa Idara ya Bima wa Benki ya Biashara ya Taifa TCB  Francis Kaaya 

Wed, 25 Aug 2021 Chanzo: millardayo.com

Vikundi mbalimbali vilivyosajiliwa na visivyosajiliwa nchini vimeshauriwa kuchangamkia fursa ya huduma ya  bima ijulikanayo kama NISHIKE MKONO inayotolewa na benki ya taifa ya Biashara TCB  ili kuwawezesha kujipatia fidia pale wanapopatwa na majanga.

Akizungumza mkoani Dar es salaam Mkuu wa Idara ya Bima wa Benki ya Biashara ya Taifa TCB  Francis Kaaya  amesema benki ilianzisha huduma ya Bima ya nishike mkono ambayo hivi sasa  imeboreshwa kwa kuongeza wanufaika ikiwemo watoto wanne na wakwe.

“Tumeboresha fao tulilokuwa tunatoa mwanzo, ilikuwa Shilingi 2000 kwa mwezi, ikiwa Mwananchama akifariki itatolewa Milioni 5, akifiwa na mwenza tutampa Milioni 4, tumeongeza Wazazi na wakwe, akifiwa na Mkwe tunatoa Milioni 1 pia akifiwa na Mzazi wake Milioni 1” Mkuu wa Idara ya Bima wa Benki ya Biashara ya Taifa TCB  Francis Kaaya

“Tumeongeza pia kwa upande wa Watoto ikiwa Mwananchama amefiwa na Mtoto wasiozidi wanne, mtoto chini ya miaka 21 atapewa Milioni 2 kwa kiasi cha 2000 kwa mwezi” Mkuu wa Idara ya Bima wa Benki ya Biashara ya Taifa TCB  Francis Kaaya

“Vile vikundi vilivyojiunga mwanzo vitafaidika na fao hili bila kuongeza chochote, watu wajiunge, tunalipa ndani ya Saa 72” Mkuu wa Idara ya Bima wa Benki ya Biashara ya Taifa TCB  Francis Kaaya

Chanzo: millardayo.com