Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakumbushwa kufanya shughuli mita 60 toka chanzo cha maji

Cfeac3d1d4093fefb484cca112762f56 Wakumbushwa kufanya shughuli mita 60 toka chanzo cha maji

Tue, 4 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WANANCHI wanaoishi kwenye Bonde la Ziwa Victoria na maeneo mengine ya nchi wamekumbushwa kuacha umbali wa mita 60 kutoka chanjo za maji chochote kilicho karibu yao kwa sababu maji huwa hayasahau mkondo wake na ipo siku yatarudi na kuleta maafa.

Hayo yamebainishwa kwenye Maonesho ya Wakulima ,wafugaji na wavuvi yanayoendelea kitaifa mkoani Simiyu katika viwanja vya Nyakabindi mjini hapa na Mhandisi Rasilimali za Maji wa Bodi ya Maji ya Bonde la Ziwa Victoria, Migalu Mollel.

Alisema maji ni rasilimali muhimu katika uhai na kwenye shughuli zote za kilimo,ufugaji na uvuvi na kwamba kama hakutakuwa na mpangilio mzuri wa utunzaji vyanzo hivyo uchafuzi na uharibifu unaweza kuleta madhara na kuharibu ikolojia.

Mollel alisema katika maonesho hayo yameshiriki kwani wao ni wadau wakubwa na wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhakikisha wanafuata sheria ikiwemo hiyo ya kukaa au kufanya shughuli mbalimbali nje ya Mita 60 kutoka chanzo cha maji.

“Tunaendelea kuwaelimisha wananchi kuhakikisha wanatekeleza ile sheria inayowataka kukaa umbali wa mita 60 kutoka chanzo cha maji kwani wasipotii maji huwa hayasahau mkondo ipo siku yatarudi na kuleta maafa”,alisema Mollel.

Alitoa mfano kwamba mwaka 2019/2020 umekuwa ni mwaka uliopata mvua nyingi zilizovunja rekodi ya kuwa na kina cha juu cha maji kilichofika Mita 1,134.85 kutoka usawa wa bahari rekodi ambayo iliwahi kutokea mwaka 1965 kwa kurekodi kiwango cha maji Mita 1,134.27.

Alisema kutokana na nchi kupata mvua za kutosha wananchi ambao walikiuka sheria na kufanya ujenzi au shughuli ndani ya mita 60 kutoka chanjo cha maji,wamekumbwa na mafuriko na kuwataka kuhama na kutii sheria.

Akizungumzia kiwango cha maji kilichopo katika Ziwa Victoria kama kina kidhi mahitaji ya watumiaji,Mollel alisema yapo ya kutosha na kuwataka watumiaji wakiwemo wafugaji ambao baadhi yao wanaharibu vyanzo hivyo kwa kuingiza mifugo,kuacha na kufuata taratibu za matumizi ya maji.

Chanzo: habarileo.co.tz