Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakulima waomba serikali kuboresha kilimo cha umwagiliaji

Ab0fab1cdafd780355a78425a0fdf83c Wakulima waomba serikali kuboresha kilimo cha umwagiliaji

Fri, 22 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WAKULIMA wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma wameomba serikali kuboresha kilimo cha umwagiliaji kwa kuwa ndicho kinachompa mkulima uhakika wa kuvuna hata kama mvua zitakuwa chache.

Wakizungumza katika mahojiano,mmoja wa wakazi wa kijiji cha Mbori wilaya Mpwapwa ,Magreth Samson alisema kilimo cha umwagiliaji ndicho kilimo chenye uhakika.

Alisema serikali na wakulima waunganishe nguvu katika kutatua changamoto za uendeshaji wa kilimo cha umwagiliaji pamoja na masoko ,viuatilifu na uharibifu wa mazingira.

Magreth ambae ni binti aliyejikita kwenye kilimo cha matunda aina ya matikiti alisema serikali ikisaidia kupunguza changagoto hizo na kuboresha mifumo ya umwagiliaji hasa sehemu za vijijini vijana wengi watahamsika kujikita katika kilimo .

Alisema kwa sasa Tanzania idadi kubwa ya Watanzania wanajihusisha katika kilimo lakini bado miundombinu yake haijaboreshwa na hivyo kujikuta wanafanya kilimo cha kujikimu.

Mkulima mwingine John Lugendo alisema uharibifu wa mazingira unahatarisha kilimo endelevu na kutishia kupoteza mitaji.

Lugendo alisema kwa kushirikiana na Chama cha Kilimo cha Bustani cha Tanzania (TAHA) wameweza kulima kilimo cha umwagiliaji lakini wanakabiliwana changamoto nyingi ikiwamo viuatilifu feki.

Ofisa wa Umwagiliaji TAHA, Philip Shimba alisema lazima wakulima wataona faida kwa kilimo wanachokifanya endapo watazingatia maelekezo ya watalamu na kuachana kilimo cha mazoea.

Shimba alisema changamoto kubwa anayokabili ni wananchi kuto zingatia maelezo wanayopewa na watalaamu kwa kisingizo cha ukosefu wa mitaji.

Ofisa kilimo,umwagiliaji na ushirika wa Wilaya ya Mpwapwa Maria Lesharu amekiri kuwepo kwa changamoto ya uharibifu wa mazingira katika bonde la Mbori na Tambi kitu alicho kisema kuwa tayari wameshaunda kamati za mazingira za kata ili kuweza kuthibiti uharibifu kuanzia ngazi ya vijiji hadi wilaya.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mpwapwa, Jabir Shekimweri alisema kuna changamoto kubwa ya uharibifu wa mazingira katika wilaya yake na wanachukua hatua ya kukabilina na hali hiyo.

Chanzo: habarileo.co.tz