Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakulima wadogo wanawake watoa kilio chao cha mitaji

174ea573e6fffe10ebe2aeff210be21b.jpeg Wakulima wadogo wanawake watoa kilio chao cha mitaji

Sat, 28 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WAKULIMA wadogo wanawake wameitaka serikali wakati wanakamilisha sera ya kilimo, taratibu na mifumo kuhakikisha kwamba inawasaidia wanawake ambao hujishughulisha na kilimo vijijini.

Aidha imeelezwa kuwa pamoja na kuwa na mchango mkubwa katika uchumi wa taifa, wanawake wakulima vijijini wamekuwa wakisumbuka na upatikanaji wa mitaji na soko lenye uhakika wa mazao yao.

Aidha kutokana na kukosa maarifa mapya wamekuwa wakitumia pembejeo mbalimbali bila utaratibu unaotakiwa na kusababisha hasara kubwa.

Aidha lipo tatizo la teknolojia ya uhifadhi ambalo inasababisha uwapo wa sumu kuvu katika mazao kutokana na wao kushindwa kuhifadhi mazao hayo kwa namna inavyotakiwa.

Hayo yote yamesemwa katika mkutano maalumu wa wakulima wadogo wapatao 90 kutoka mikoa mbalimbali waliokuwa wakijadiliana changamoto zinazowakabili wakulima wadogo wanawake nchini na namna ya kukabiliana nazo.

Mkutano huo umeandaliwa na Jukwaa la Wakulima Wanawake Vijjini (RWFF).

Mkutano huo ambao ulifadhiliwa na Action Aid Tanzania, ulihudhuriwa pia na wawakilishi kutoka Wizara ya Kilimo na vyama mbalimbali vya kiraia.

Lengo kuu la mkutano huo kwa mujibu wa Rais wa Jukwaa hilo, Amina Senge ni kutafuta maoni ambayo yataingizwa katika mpango wa maendeleo wa sekta ya kilimo wa 2021 hadi 2026.

Alisema kwamba wanawake wengi wanakabiliwa na matatizo lukuki katika kuendesha kilimo chao hasa upataji wa mitaji ya kuimarisha kilimo.

Alisema wakati umefika kwa Wizara ya Kilimo kufanya kazi karibu zaidi na wakulima wadogo wanawake kuanzia ngazi za chini ili kuimarisha tija na kuleta kipato kwa taifa.

Rais wa Jukwaa la Wakulima Wanawake la Afrika, Eva Mageni amewataka wanawake wakulima wadogo wa Tanzania kutumia jukwaa lao vyema ili kuweza kufikisha mahitaji na matarajio yao serikalini.

Magreth Thomas, mmoja wa wakulima wadogo kutoka Mkoa wa Morogoro aliitaka serikali kuhakikisha kwamba inapeleka maofisa ugani vijijini kusaidia kuwapa maarifa wanayohitaji ili kukuza kilimo chao.

Jukwaa hilo lenye wanachama 28,343 kwenye vijijini 820 ndani ya wilaya 28 nchini lilianzishwa mwaka 2017 kwa lengo la kuwapa uwezo wakulima wadogo wanawake kufahamu haki zao na kushiriki katika maamuzi makubwa ya kitaifa ambayo nao yanawahusu.

Chanzo: habarileo.co.tz