Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakulima wa korosho wakopeshwa pembejeo

KOROSHO Wakulima wa korosho wakopeshwa pembejeo

Mon, 22 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WAKULIMA wa Korosho wa Chama cha Ushirika cha MAMCU, wamekopeshwa pembejeo za kilimo zaidi ya tani 1,500 za salfa ya unga.

Lengo la kukopeshwa ni kuhakikisha kuwa wanaongeza tija ya uzalishaji wa korosho kwa msimu wa 2020/2021.

Wakulima hao walipatiwa mkopo huo jana wilayani Masasi, baada ya chama hicho kuzindua rasmi mchakato wa ugawaji wa pembejeo za kilimo kwa mkopo kwa wakulima wake kupitia vyama vyao vya ushirika vya msingi.

Akisoma taarifa ya ugawaji wa pembejeo hizo, Meneja wa MAMCU tawi la Masasi, Joseph Mmole, alisema katika kuelekea msimu mpya wa zao hilo la korosho, MAMCU kimeamua kuwapatia mkopo wa pembejeo za kilimo wakulima wake ambayo ni salfa ya unga kwa bei ya Sh.32,000 kwa mfuko mmoja.

Alisema hadi sasa tayari wameshasambaza kilogramu 699,000 ambayo ni sawa na mifuko ya Salfa 27,960 kwenye vyama vya msingi vya ushiria 72 ambavyo ni wanachama wao.

Alisema moja ya faida ya mkopo huo kwa wakulima ni kwamba mkulima atafanya marejesho ya fedha baada ya mauzo ya korosho zake katika msimu huo.

“Matarajio yetu hadi kufikia mwishoni mwa mwezi huu tutakuwa tayari tumeshamaliza kusambaza pembejeo zote kwa wakulima kupitia kwenye vyama vyao vya ushirika,”alisema Mmole.

Alisema vyama vya msingi vya ushirika 72 watanufaika na mkopo huo.

Mwenyekiti wa MAMCU mkoa wa Mtwara, Joseph Kidando, aliwataka wakulima hao kutambua kuwa pembejeo hizo siyo zawadi, bali wazitumie kwa malengo yaliyokusudiwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live