Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakulima wa Kitunguu walia na ugonjwa wa kaukau

Zzx Wakulima wa Kitunguu walia na ugonjwa wa kaukau

Tue, 6 Apr 2021 Chanzo: ippmedia.com

Hatua hiyo imekuja baada ya takribani zaidi ya hekta 17 za kitunguu kuathiriwa na ugonjwa huo licha ya juhudi za wakulima kutumia kila aina ya dawa na kushindwa kupatikana suluhu ya ugonjwa huo.

Bwana shamba katika kata hiyo, Juma Shabani, ameliambia Nipashe kwa njia ya simu kuwa wamejitahidi kadri ya uwezo wao lakini wameshindwa kupata suluhu na badala yake wameiomba serikali kuingilia kati kuleta wataalam.

"Ugonjwa huu wa kaukau umekuwa tishio Sana kwa zao hili la Kitunguu mwaka huu kila kona kwa wakulima hapa Ruaha Mbuyuni kilio ni hicho hicho watu wamewekeza katika ardhi lakini wameambulia patupu" 

Alisema zaidi ya hekta kumi na Saba mwaka huu zimekumbwa na janga Hilo na ugonjwa huu unasambaa kwa kasi zaidi na badae utakuwa janga la nchi nzima kwa wakulima wa kitunguu hivyo jitihada za lazima zinahitajika kutoka kwa Serikali ili kuwakomboa wakulima hawa.

Aliongeza walishapeleka sampo katika vyuo vya utafiti (SUA) na Uyole vilivyopo Mbeya  kwa mda mrefu lakini bado hawajarejesha majibu kujua ni sawa gani ya kutumia.

Kwa upande wake Fundi Pikipiki katika kata hiyo ya Ruaha Mbuyuni, ambaye pia ni muhanga katika janga hilo Maonezi Mohamedi, ameiomba serikali kuongeza jitihada za lazima kuwanusuru wakulima  hasa wanapoanza msimu huu mpya wa Kilimo

"Kwa sasa tunaanza msimu mpya tena wa kilimo na wakulima wamekata tamaa kwa kuhofia ugonjwa huo korofi shambani mwaka jana nililima heka tano sijaambulia chochote baada ya kuingiliwa na ugonjwa huo"

Naye Halima Ngambi, ambaye pia ni mkazi wa kata hiyo ya Ruaha Mbuyuni, alisema ugonjwa ulipoingia ulikuwa hauna madhara makubwa sana lakini kwa sasa umekuwa na madhara makubwa na hata Kitungu kilichoharibiwa na ugonjwa huu kimekosa  kwa sababu kinanyongea kinakuwa chembamba kama ukenge, alisema 

Chanzo: ippmedia.com