Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakulima Ruvuma washauriwa kuchangamkia miche ya kahawa

92d35603041d4027070f7042dd65843b Wakulima Ruvuma washauriwa kuchangamkia miche ya kahawa

Mon, 10 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WAKULIMA wa Mkoa wa Ruvuma wametakiwa kuchangamkia fursa ya miche ya kahawa kwa sababu maeneo mengi ya mkoa yanafaa kwa kilimo cha zao hilo ambalo limeinua maisha ya watu wengi kiuchumi.

Wito huo umetolewa na mtaalamu wa kilimo, Victor Akulumuka kutoka Kituo cha Utafiti wa zao la Kahawa(Tacri)cha Ugano wilaya ya Mbinga katika maonesho ya Wakulima na Wafugaji yaliyofanyika viwanja wa Msamala mjini Songea.

Akulumuka alisema wakulima wanatakiwa kuchangamkia fursa ya kulima zao la kahawa kwa kuwa linaonekana kustawi katika maeneo mengi ndani ya mkoa na kilimo ambacho kitainua uchumumi wao na taifa.

Aliwataka wakulima kuzingatia amri kumi za kilimo cha kahawa ambazo zinasaidia katika kustawisha zao la kahawa ambazo zitatoa matokeo chanya na kuongeza uzalishaji wenye tija kwa wakulima .

Alizitaja amri za kilimo bora cha kahawa kuwa ni kukatia matawi, kutumia mbolea,kupulizia dawa kwa wakati, kupalilia na kuondoa machipukizi. Kupanda miti kwa ajili ya kutunza ubaridi katika shamba.

Aidha alisema endapo wakulima watafuatilia na kusimamia na kufuatilia kilimo cha kahawa mkulima anaweza kuvuna kilo tatu kwa shina moja, ambapo kwa ekari moja mkulima anaweza kuvuna kilo zaidi ya 1,500 kutokana na shamba lenye ukubwa wa ekari moja ambapo hupandwa miche 540.

Chanzo: habarileo.co.tz