Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakorea kujenga mji mpya Toangoma, mabondeni kutengewa viwanja

58368 Pic+wakorea

Mon, 20 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Halmashauri ya Manispaa ya Temeke  imesaini mkataba wa ujenzi wa mji wa kisasa uliopo eneo la Vikuani Toangoma na Kampuni ya Dohwa ya Korea Kusini, utakaogharimu Sh1.8 bilioni.

Akizungumza baada ya kusaini mkataba huo leo Jumamosi Mei 19, 2019 Mkurugenzi wa manispaa ya hiyo, Ludubilo Mwakibibi, amesema mradi huo unatarajiwa kukamilika kwa miezi sita vitapimwa viwanja vya makazi eneo la Vikunai Toangoma kuanzia 400 hadi 600.

Mwakibibi amesema kampuni hiyo itaandaa michoro ya mipango miji, itapima ardhi, itaandaa hati za umiliki, kuandaa michoro ya usanifu wa uendelezaji ujenzi katika eneo hilo.

"Kazi yetu ni kutekeleza kwa vitendo, hivyo tunawaomba wananchi wetu siku tutakapotangaza wajitokeze kwa wingi kununua kwa kuwa atakapokabidhiwa atapewa na hati miliki,” amesema.

 

Naye Meya wa manispaa ya hiyo, Abdallah Chaurembo, amesema mradi huo unatekelezwa kupitia Mradi wa Maendeleo Endelevu wa Jiji la Dar es Salaam (DMDP)  kwa manispaa za Dar es Salaam.

Pia Soma

Amesema mradi huu utatekelezwa kwa kuzingatia sheria za ununuzi, amewataka wananchi na watumishi wa umma kuchangamkia fursa hiyo.

"Tunataka watu waishi kwa mchanganyiko. Naomba mkurugenzi utenge maeneo ya watu wanaokaa maeneo hatarishi kwa ajili Dar es Salaam tuwape hata watu wanaotoka Manispaa ya Ilala na sehemu zingine," amesema Chaurembo.

 

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz