Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakili Madelea kusomewa upya mashtaka ya utakatishaji fedha

Madeleka Pic Data Wakili Madelea kusomewa upya mashtaka ya utakatishaji fedha

Tue, 18 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imetengua makubaliano ya Plea Bargain aliyoingia wakili Peter Madeleka na ofisi ya mwendesha mashtaka wa Serikali DPP baada ya Wakili huyo kuyakatia rufaa.

Mahakama kuu chini ya Jaji A. Bade imesema makubaliano hayo yaliyofanyika chini ya Mahakama ya Hakimu mkazi Arusha kufuatia kesi ya uhujumu uchumi namba 40 ya mwaka 2020 ni batili na imeamuru kesi hiyo ianze upya.

Kufuatia maamuzi hayo wakili Peter Madeleka amekamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi huku akisubiri kesi hiyo kuanza upya na kwa kuwa moja ya makosa yanayomkabili ni utakatishaji fedha ambayo haina dhamana, hivyo basi wakili huyo atakuwa mahabusu wakati kesi yake ikiwa inaendelea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live