Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakazi wa mabondeni wakesha wakihofu mafuriko Dar

Mabondeni Mvua Mvua.png Wakazi wa mabondeni wakesha wakihofu mafuriko Dar

Thu, 2 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam zimekuwa kilio kwa wakazi wake kutokana na adha wanayoipata kutokana na baadhi ya maeneo kujaa maji na kusambaa takataka.

Hayo yanathibishwa na baadhi ya wamiliki wa vyombo vya usafiri na watembea kwa miguu wanaodai maeneo mengi yamejaa maji ikiwepo mabondeni na barabara za mtaani.

Mvua hizo zimeanza kunyesha Oktoba 31, 2023 zimeleta madhara kwa wakazi wa jiji hili ikiwemo kushindwa kufika katika shughuli mbalimbali.

Wakizungumza changamoto hizo baadhi ya wakazi wa bondeni na wafanyabiashara wamedai kuwa mvua hizo zimesimamisha baadhi ya shughuli zao kwa kuhofia nyumba zao kujaa majani kutokana na taarifa za utabiri uliotolewa.

"Sisi wakazi wa bondeni tunalala kwa wasiwasi kwa kuhofia maji kujaa kwenye nyumba zetu, tunakesha kujaza michanga ili kuzia maji," Khadija Ali mkazi wa Kawe Mnarani.

Hoja hiyo imeungwa mkono na Amos Kazikazi mbeba michanga katika eneo la Mto Mbezi amesema kwa sasa wakazi wa bondeni wanakaa macho kuhofia maji na wao kutakiwa kubeba michanga kutoka kwenye mto wakati maji yakiendelea kusogea.

"Nimeamaka tangu asubuhi nabeba michanga napeleka kwenye nyumba huko juu hapa natembea kwa tahadhari kuhofia kuondoka na maji licha ya kupata fedha lakini kuna haja ya Serikali kufanya jambo kuwatoa hawa watu wanaishi sehemu hatarishi," amesema Kazikazi.

Omary Pambe ambaye ni dereva wa pikipiki amesema hali ya hiyo imewakosesha abiria kwa kuwa wateja wao wengi ni wafanyabiashara wa sehemu mbalimbali ikiwepo Mwenge ambao kukiwa na mvua wanakaa nyumbani kwa madai hakuna wateja.

"Abiria ninaowapakia wanafanya shughuli zao mwenge kukiwa na mvua wanasema hakuna biashara hivyo wanalala nyumbani, abiria tunaowapata wanasema hatuna vikinga mvua hataki kuloana,"amesema Pambe.

Andrew Kilangi ambaye ni mwanafunzi wa Sekondari Makongo, amesema kwa kipindi cha mvua hawezi kwenda shule kutokana na njia anazopita zinajaa maji hivyo hubaki nyumbani na inapotokea kuna mitihani huamia kwa rafiki zake ili afike shule.

"Mvua ikinyesha mfululizo siwezi kwenda shule kutokana na hali ya njia ya kwetu siku muhimu kwetu ni kipindi cha mitihani ndiyo naongea na wazazi nilale kwa rafiki zangu hadi nitakapomaliza mitihani narudi, huruma kipindi cha mitihani ya Taifa kama kwa sasa kidato cha pili wapo kwenye mitihani," amesema Kilangi.

Katika maeneo ya Posta barabara zote zinapitika ikiwepo eneo la Chuo cha Biashara (CBE) ambapo imekuwa ikifahamika kuwa ni eneo linalojaa maji siku zote inaponyesha mvua.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live