Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakazi wa Jimbo la Makete waomba Barabara

75c1121172c20b8b2de274fcb51b6650 Wakazi wa Jimbo la Makete waomba Barabara

Fri, 4 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Wananchi wa Wilaya ya Makete wameiomba Serikali kutenga bajeti ya kujenga barabara ambazo zitapitika wakati wote wa mvua na kiangazi kwani barabara ndiyo zimeshika uchumi wao wa kifedha kwani mazao yao ya kibiashara wanayolima wanategemea zaidi kuuza nje ya wilaya yao.

Hayo wamesema baada ya wananchi wa kijiji cha Lugoda ambao walichanga hela kushirikiana na Mbunge wa jimbo la Makete Festo Sanga ili kukodi katapila la Halmashauri kuchonga barabara ziweze kupitika baada ya kuharibika hali inayosababisha usumbufu kwa wagonjwa ambao wanatakiwa kuwaishwa hospitali na kusafirisha mazao kutoka vijijini kwenda nje ya wilaya.

Mmoja ya wananchi wa kijiji hicho Toweni Mkwama amesema kwasasa wanauza mazao kwa bei ndogo kwasababu ya kutokuwepo kwa barabara nzuri hali inayowapelekea wafanyabiashara wa kununua mazao kuwashushia bei wakidai ubovu wa barabara unapandisha gharama ya usafirishaji wa mazao.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la makete Festo Sanga ameiomba serikali kuangalia tatizo la barabara katika jimbo hilo ambalo linatatizo kubwa la miundombinu mibovu ya barabara na hatamani kama mbunge kuona wananchi wake wanateseka kwasababu ya ubovu barabara

"Sisi makete changamoto yetu ya kwanza ni barabara kwasababu sisi tunamsimu mrefu wa mvua hunyesha kwa miezi isiopungua 8 hivyo huitaji wa barabara ni mkubwa sana,tunaomba serikali kuongeza fedha ili TARURA wapate fedha nyingi kujenga barabara, lakini pia TANROAD wapewe fedha za kibajeti walizoomba ili watusaidie barabara zetu zipitike."Mbunge wa makete

Chanzo: habarileo.co.tz