Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakazi wa Dar es salaam watakiwa kujitokeza upimaji magonjwa ya moyo

0731b2bd0aacaa59bd3b60eb02c6f1c9 Wakazi wa Dar es salaam watakiwa kujitokeza upimaji magonjwa ya moyo

Thu, 4 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WAKAZI wa Mkoa wa Dar es Salaam na mikoa ya jirani, wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika upimaji na utoaji wa elimu ya magonjwa ya moyo litakalofanywa kwa siku mbili kuanzia kesho kwa kushirikiana na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Madaktari bingwa wa magonjwa ya wanawake.

Upimaji huo ambao utakwenda sambamba na maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyoanza Machi 2, na itafikia kilele chake Machi 8, utafanyika kwa watoto na watu wazima katika viwanja vya Zakheem Mbagala jijini Dar es Salaam kuanzia saa 2:00 asubuhi.

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano JKCI, Anna Nkinda alisema watu wengi wanasumbuliwa na magonjwa ya moyo hasa shinikizo la juu la damu pasipo kujijua na kuwasisitiza wananchi kutumia nafasi hiyo kupima afya zao.

Alisema ugonjwa wa shinikizo la juu la damu unaua polepole na asilimia 90 ya wagonjwa ambao wanakutwa na ugonjwa huo wanatakiwa kutumia dawa muda wote wa maisha yao.

“Kwa wale watakaokuwa na matatizo ya moyo watafanyiwa uchunguzi zaidi na kupatiwa matibabu au kushauriwa rufaa ya kuja kwenye hospitali ya JKCI kwa ajili ya matibabu ya kipingwa zaidi,” alisema

Kaulimbiu ya mwaka huu ya Siku ya Moyo Duniani ni Wanawake na Uongozi, Chachu ya kufikia dunia yenye usawa

Chanzo: www.habarileo.co.tz