Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakazi Nyamongolo watakiwa kupima maeneo yao

0aa5912580d4082e8dfbac0a421074d3 Wakazi Nyamongolo watakiwa kupima maeneo yao

Tue, 13 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MGOMBEA ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk Angelina Mabula amewataka wakazi wa kata ya Nyamongolo kuhakikisha wanapima maeneo yao ya ardhi na kuweza kuchukua hati yao.

Rai hiyo ilitolewa wakati wa mkutano wake wa 36 wa kampeni katika viwanja vya shule ya msingi Nyamadoke.Alisema katika kata hiyo tayari viwanja 7426 vimepimwa na wakazi waliochukua hati ni 816.

Dk Mabula alisema tayari nyumba sita za polisi wamejenga katika kata hiyo nab ado watajenga nyumba sita zingine. Aliahidi kukamilisha ujenzi wa kituo cha polisi kwenye kata hiyo.

Dk Mabula aliwahidi wakazi wa Nyamongolo kuwajenga barabara za lami katika njia ya Buswelu kwenda Nyamadoke na tayari milioni 45 imetengwa. Alisema njia nyingine itakayowekewa lami ni Nyamngolo viwanda kwenda center na tayari milioni 27 imetengwa.

Chanzo: habarileo.co.tz