Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakazi Dar kupata msaada wa kisheria

94054 Pic+sheria Wakazi Dar kupata msaada wa kisheria

Mon, 3 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Paul Makonda amezindua siku tano za maadhimisho ya wiki ya sheria na kuwataka wananchi kufika viwanja vya Mnazi Mmoja kupata msaada wa kisheria.

Akizungumza leo Jumamosi  Februari Mosi, 2020 katika  maadhimisho ya wiki ya sheria itakayohitimishwa na kilele cha siku ya sheria, Makonda amesema wananchi wenye matatizo ya kibiashara, migogoro ya ardhi na mirathi watasaidiwa.

Amesema katika maadhimisho hayo yanayofanyikwa viwanja vya Mnazi Mmoja kutakuwa na maofisa wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita), Jeshi la Polisi, Magereza na ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka (DPP).

"Wale waliokuwa wakija ofisini kwangu wanalalamika nawasihi waje katika viwanja vya mnazi mmoja ili mpate elimu haki zenu,” amesema Makonda.

Naye Jaji mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Lameck Mlacha amewataka wananchi kujitokeza  kwenye viwanja hivyo kwa sababu watapokea kero zao na kuwapa msaada wa kisheria.

Chanzo: mwananchi.co.tz