Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakala,Tanesco waeleza tembe kufungwa umeme

49746 Pic+umeme

Mon, 1 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kaimu mkurugenzi mkuu wa Wakala wa Umeme Vijijini (Rea), Amos Maganga, amesema zipo nyumba za tembe ambazo zinaweza kuunganishiwa umeme baada ya kujiridhisha kwamba zina usalama wa kutosha.

Maganga aliyasema hayo jana akizungumza na Mwananchi baada ya picha ya nyumba ya tembe iliyounganishiwa umeme kuibua mjadala kwenye mitandao ya kijamii huku baadhi ya watu wakigusia suala la usalama wa wananchi na aina ya nyumba zinazostahili kupata huduma hiyo.

Maganga alisema nyumba hizo zinaunganishiwa umeme baada ya wataalamu kujiridhisha kwamba kuna usalama wa kutosha.

Alisema jambo muhimu ni uwekaji wa vifaa vya kiusalama kwenye nyumba iliyounganishwa umeme.

Hata hivyo, Maganga alisema Rea wanafanya kazi kulingana na viwango (specifications) vya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na kusisitiza wao ndiyo wanaweza kulizungumzia zaidi suala hilo.

Naye meneja uhusiano wa Tanesco, Leila Muhaji, alisema nyumba hizo zinafungwa kifaa kinachoitwa Umeme Tayari (ready board).

Muhaji alisema kifaa hicho kinafungwa kwenye nyumba ambazo hazina mtandao mkubwa wa umeme (wiring) na nyumba hizo huwa na chumba kimoja au viwili. Amesema kifaa hicho kinakuwa na mfumo wa usalama ndani yake.



Chanzo: mwananchi.co.tz