Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakabidhiwa bweni la wanafunzi 240 wa kike

Gtfxrezxfcf Wakabidhiwa bweni la wanafunzi 240 wa kike

Tue, 28 May 2024 Chanzo: Mwananchi

Takribani wanafunzi 240 wanawake katika Shule ya Sekondari Namanga, wameepukana na safari ya kutoka nyumbani kwenda shule, badala yake wataanza kuishi bweni.

Hatua hiyo ni baada ya shule hiyo kukabidhiwa jengo la bweni litakalolaza wanafunzi 240, kutoka kwa Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Huduma za Kisheria (LSF).

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi jengo hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa LSF, Lulu Ng'wanakilala amesema dhamira yao ni kuboresha miundombinu ya shule.

Lengo lingine la msaada huo walioutoa kwa kushirikiana na North-South Cooperation kutoka Luxemburg, unalenga kuwawezesha wanafunzi, hasa wasichana, kupata haki yao ya elimu bora.

"Mradi unashughulika na mila potofu zinazowakandamiza wanawake na wasichana na kupambana na ukatili wa kijinsia katika jamii.

“Aidha, mradi huu unalenga kuwawezesha wasichana kutimiza ndoto, kuhakikisha usalama wao dhidi ya ukatili wa kijinsia wakiwa shuleni na kukuza uendelevu wa mazingira kwa kupanda miti," amesema.

Ameeleza bweni hilo litawapa wanafunzi hao mazingira mazuri ya kujifunza.

Meneja Mkuu wa North-South Cooperation, Roberto Marta, amesema ni miaka miwili sasa tangu washirikiane na LSF na bweni hilo ni moja ya matunda.

“Tunafurahi kuona wasichana wa Kimasai sasa watakuwa na mazingira mazuri ya kusomea. Serikali ya Luxemburg inajivunia kuunga mkono miradi inayoboresha maisha ya kijamii na kiuchumi,” amesema.

Mkuu wa Wilaya ya Longido, Marko Ng'umbi amesema jengo hilo linaibua matumaini na fursa kwa wanafunzi kujisomea katika mazingira bora na rahisi.

"Juhudi hii bila shaka itakuwa na alama ya kudumu katika maisha ya vijana wetu, ikiwapa mazingira wanayohitaji ili kufaulu katika masomo yao na kufikia ndoto zao,” amesema.

Chanzo: Mwananchi