Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wajawazito wawili walalia kitanda kimoja hospitali ya Katoro

Wajawazito Pic Nbnb Wajawazito wawili walalia kitanda kimoja hospitali ya Katoro

Fri, 4 Nov 2022 Chanzo: mwanachidigital

Wingi wa wanawake wanaojifungua kwenye kituo cha afya Katoro umesababisha baadhi yao kulala wawili wawili kitanda kimoja.

Kutokana na changamoto hiyo halmashauri ya Geita imeongeza vitanda 20 kwenye kituo hicho na kufanya uamuzi wa kubadili wodi iliyojengwa kwa ajili ya wanaume itumike na wanawake ili kupunguza msongamano huo.

Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo, Modest Burchard amesema kituo cha afya Katoro kinawahudumia wakazi 180,000 wa mji mdogo Katoro idadi mbayo ni kubwa na inaongeza msongamano wa wagonjwa kwenye kituo hicho.

Amesema kwa mujibu wa Muongozo wa Wizara ya afya Kituo cha afya kinapaswa kuwa na vitanda 50 pekee, lakini kutokana na ongezeko la wagonjwa kwenye kituo hicho kwa sasa kitakuwa na vitanda 86 huku wodi ya kina mama wanaojifungua yenye vitanda 30 sasa kuwa na vitanda 50.

“Idadi hii ya wanawake 40 kujifungua kwa siku moja inazidi hata hospitali za rufaa au mkoa, wodi yetu hapa ina vitanda 30 wanapojifungua 40 kwa siku moja inawalazimu wengine kulala wawili.

“Vitanda hivi tunaangalia namna ya kuvipeleka kwenye wodi nyingie itakayotumiwa na wanawake wanaojifungua ili kupunguza msongamano kwenye wodi mama inayotumika sasa.

“Serikali imeona na inajua kituo hiki kimelemewa na ndio maana imetoa fedha kwa ajili ya Hospitali ya Katoro itakayokuwa na hadhi ya hospitali ya wilaya ujenzi unaendelea na mwakani Januari tunategemea inaze kutumika,” amesema.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo John Wanga akikabidhi vitanda hivyo vyenye thamani ya Sh 14milioni amesema serikali imesikia kilio cha wanawake wanaolazimika kulala wawili kwenye kitanda kimoja.

“Tumeagiza vitanda 50 kwa sasa tumepokea 20 tumeona tuvilete ili kupunguza msongamano kituo hiki kinahudumia wananchi wa Buseresere, Rwamgasa, Kaseme na kata nyingine na hii ndio inaleta changamoto ya msongamano kwa kina mama wanaojifungua,” amesema.

Chanzo: mwanachidigital