Mkuu wa wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza Ng’wilabuzu Ludigija amewataka wanawake wilayani humo kuacha tabia ya kunywa dawa za mitishamba pindi wanapokuwa wajawazito na badala yake waende hospitali ili kupata huduma sahihi na hatimaye wajifungue Watoto wenye afya.
Ludigija ametoa kauli hiyo wakati akizindua huduma za afya katika zahanati ya Sangu iliyopo katika Kijiji cha Sangu kata ya Mhande na kuwataka wakazi wa Kijiji hicho kutunza miundombinu ya zahanati hiyo ili iwasaidie kupata huduma za afya.
niwasihi wananchi inawezekana mmesubiri kwa muda mrefu kupata zahanati hii sasa mmepata itumieni vizuri wataalamu wa afya wapo niwaombe mtoe ushirikiano kwao na hasa wanawake hatutarajii kusikia mnajifungulia nyumbani mana huduma imesogezwa karibu vilevile achene kutumia dawa za mitishamba mkiwa wajawazito maana ni hatari kwa mtoto aliyepo tumboni’
Katika hatua nyingine Dc Ludigija amewataka wakazi wa wilaya hiyo kuhakikisha wanalala kwenye chandarua ili ili kujikinga na ugonjwa wa maralia.