Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wajanja waingiza mifuko isiyo rafiki kwa mazingira

60282 Pic+plastic

Thu, 30 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi. Serikali mkoani Kilimanjaro imebaini uwepo wa mifuko mbadala katika mzunguko ambayo malighafi zake zina plastiki, tofauti na maelekezo ya Serikali ya aina ya mfuko mbadala inayokubalika.

Hayo yameelezwa leo Mei 29,2019 mjini Moshi na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira na kulitaka Shirika la Viwango Tanzania (TBS),  kuweka bayana juu ya viwango vya mifuko mbadala inayokubalika.

Mbali na changamoto hiyo, lakini mkuu huyo wa mkoa amesema imejitokeza changamoto nyingine kwa wauzaji wa nyama katika mabucha kutumia magazeti kufungia nyama.

Kutokana na hali hiyo, amepiga marufuku matumizi ya magazeti kufungia nyama, na akawataka wenye mabucha kuwasiliana na wazalishaji wa mifuko mbadala ili wawapatie mifuko ya khaki.

Pia,   mkuu huyo wa Mkoa amewataka wafanyabiashara wenye viwango vikubwa vya mifuko ya plastiki, kuisalimisha katika ofisi za halmashauri kabla ya Mei 30, 2019 ambapo matumizi yale yanafikia kikomo.

Chanzo: mwananchi.co.tz