Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wajane 300 watapeliwa fedha za kujiunga uanachama

Wajane Moro Wajane 300 watapeliwa fedha za kujiunga uanachama

Fri, 20 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha Wajane wilayani Morogoro, kimemuomba waziri wa Maendelea ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dk. Doroth Gwajima kuingilia kati swala la wajane zaidi ya 300 kutoka katika kata 10 za Manispaa ya Morogoro kutapeliwa fedha zao na mtu aliyejitambulisha mratibu wa wajane kutoka katika wizara hiyo na kudai anaendesha zoezi la usajili wa wanawake kwenye chama hicho kwa gaharama ya shilingi 3,500 na kutoa kadi feki.

Mwenyekiti wa Wilaya wa chama hicho, Loveless Kaswika amesema kuwa mtu hiyo anayetambulika kwa jina la Agatha amekuwa akiendesha zoezi hilo kinyemela katika kata hizo na kujipatia fedha isivyohalali na kusababishja usumbufu mkubwa wa wajane akidai majina hayo anayapeleka wizarani kupitia chama cha wajane taifa jambo ambalo sio kweli.

Amesema kuwa utapeli huo ulibainika baada ya badhi ya wajane kutoka katika kata mbalimbali kufika ofisini kufatilia maswali yanayo wahusu ndipo wakakutwa na kadi feki ambapo licha ya kufanya jitihada za kutaka kumkamata kwa siri mtuhumia huyo alifanikiwa kutoroka na kumuacha mmoja ya watu alikuwa akishirikiana nao katika kuandikisha na kukusanya fedha za wajane hao.

"Baada ya wajane wengi kulalamika ndipo ikabidi kumtegea mtego wa kumtaka afike mtaa wa Mkomora kata ya Maghorofani kwajili yakuandikisha wajane wengine, alikuja na moja wa watu anaoshirikiana nao lakini alipoona mimi mwenyekiti nimefika ikabidi atafute njia ya kukwepa kwamba yeye hausiki na uandikishaji baadae akatoka kama anaongea na simu na kumuacha mwezake ambaye tutamfikisha polisi" amesema mwenyekiti huyo.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hili Mwenyekiti wa Mtaa wa Mkomola, Peter Mwaipyana amesema kuwa ni kweli mtu huyo na wenzake na waliwahi kufika katika mtaa huo kwa nia ya kuandikisha wajane huku miongoni mwa vigenzo ni kupata barua ya utambulishi wa mwenyekiti ambapo licha ya kufanya jitihada za kumkamata imeshindikana baada ya kutoweka ghafa akiwa nyumbani kwake.

Jitihada za kumpata mhusika zimegongwa mwaba baada ya simu yake ya mkononi kutokuwa hewani tangu alipotoweka katika eneo la tukio.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live