Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waitara ataka utafiti kuongezeka maji ya maziwa

94a619ed9fe5b3bff732721ae72802de Waitara ataka utafiti kuongezeka maji ya maziwa

Thu, 18 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

NAIBU Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mwita Waitara ameliagiza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kufanya utafiti kuangalia namna ya kudhibiti kuongezeka kwa kina cha maji ya maziwa mkoani Singida.

Ameliagiza baraza hilo kufanya tathmini na kutoa suluhisho la kuongezeka kwa kina cha maji katika Ziwa Masogweda na Mulya katika Manispaa na Wilaya ya Singida ambayo yamefurika na kuleta madhara kwenye makazi ya watu na mashamba.

Naibu Waziri huyo alitoa agizo hilo juzi wakati wa ziara ya kikazi mkoani humo baada ya kupata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Singida, Paskasi Muragiri ambaye aliomba zichukuliwe hatua kukabiliana na hali hiyo.

Muragiri alisema ziwa hilo huenda likazingira vijiji hivyo viwili na kusababisha madhara makubwa kwa wakazi wanaoishi maeneo hayo na kumuomba Waitara kulifanyia kazi suala hilo katika ngazi ya kitaifa.

Katika ziara hiyo pamoja na mambo mengine, Waitara alitembelea machinjio katika manispaa hiyo na kuitaka halmashauri kuharakisha mpango wa kuihamishia eneo jingine walilotenga.

Pia alitembelea soko kuu na kuridhishwa na hali ya miundombinu ya kuhifadhi taka ngumu pamoja na dampo lililopo katika eneo la Manga nje kidogo ya manispaa hiyo.

Akizungumza katika kikao na maofisa mazingira kutoka manispaa hiyo, Waitara alisema ipo haja ya kuwashirikisha wananchi katika maeneo yao katika masuala ya kuhifadhi mazingira ili kupata taarifa kutoka kwenye vijiji ngazi ya chini.

Chanzo: habarileo.co.tz