Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waitara : Ilikuwa ni rahisi kufanya kazi na Rais Magufuli

428d9ed3fd03addea8f54c0451837c28 Waitara : Ilikuwa ni rahisi kufanya kazi na Rais Magufuli

Thu, 25 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mwita Waitara amemsifu Hayati Rais, Dk John Pombe Magufuli kuwa alikuwa mchapa kazi na ilikuwa ni rahisi kufanya naye kazi endapo kiongozi atafuata maelekezo yake.

Akizungumza wakati wa kutoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa Hayati Dk Magufuli, Waitara ambaye ni Mbunge wa Tarime Vijijini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliwasihi viongozi wa chama hicho kuendelea na kasi ileile ya Rais Magufuli huku akihimiza kumuunga mkono Rais, Samia Suluhu.

“Viongozi wa (CCM) wanapaswa kuhakikisha mambo ambayo Magufuli amefanya yanaendelea, sisi tutatamuunga mkono Rais Samia Suluhu,”alisema Waitara.

Waitara ambaye alikihama Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kuhamia (CCM) ameeleza kuwa Hayati Magufuli amefanya makubwa ikiwemo kutekeleza mambo mengi ambayo wapinzani walitaka yatekelezwe.

Chanzo: www.habarileo.co.tz