Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waislamu wainyoshea kidole Serikali raia kuteswa

Thu, 23 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kampala, Uganda. Mashehe na viongozi mbalimbali wa Kiislamu walitumia sherehe za swala ya Eid al-Adha kulaani mateso na matumizi ya nguvu kupita kiasi wakati wa kukamatwa kwa mwanasiasa wa upinzani na wafuasi wake wakati na baada ya uchaguzi mdogo Manispaa ya Arua wiki iliyopita.

Masaka

Sheikh wa Manispaa ya Masaka ametoa wito ufanyike mjadala kati ya serikali na upinzani ili kushusha joto la kisiasa nchini Uganda.

Akitoa mawaidha katika Msikiti Mkuu wa Masaka, Sheikh Twaha Bugembe alisema hatua za Serikali kuonyesha matumizi makubwa ya nguvu hakutaweza kurejesha amani na badala yake kutazidisha vurugu nchini.

“Pia kuna haja ya kufanyia marekebisho taratibu za uchaguzi kama ambavyo zimekuwa zikiomba asasi za kiraia, vyama vya hiari, viongozi wa dini na wanasiasa wa upinzani kwa sababu ya kuwepo vizuizi katika safari kuelekea uchaguzi huru na wa haki nchini,” alisema.

 

Gulu

Sheikh Musa Khelil wa Wilaya ya Acholi, amemtaka Rais Yoweri Museveni kumsamehe Bobi Wine aliyeko kizuizini pamoja na wanasiasa wengine wa upinzani na wafuasi wao.

Akizungumza wakati wa sherehe za Eid al-Adha katika Msikiti Mkuu wa Gulu, Sheik Khelil alisema ikiwa Serikali ilifanya majadiliano na wapiganaji waasi wa Lord’s Resistance Army, hakuna sababu kwa nini majadiliano kama yale yasifanyike hata kwa Bobi Wine na wenzake walioshtakiwa.

Viongozi wa Waislamu waliozungumzia mkasa wa kukamatwa kwa Bobi Wine na wenzake ni kutoka Kabale, Teso, Luweero, Ntungamo, Bugisu, Tororo, Mbarara.

Chanzo: mwananchi.co.tz