Katia harakati za kuhakikisha maambukizi mapya yanapungua na kufubaza makali ya Virusi Vya Ukimwi kwa wananchi, wahudumu wa Afya ngazi ya jamii wamepewa msaaada wa Baiskeli 100 kwa ajili ya kuwafikia waathirika zaidi ya elfu 80 ili waweze kupata huduma kwa muda na wakati sahihi.
Akizungumza mara baada ya kupokea Baiskeli 100 kutoka kwa shirika lisilo la kiserikali MDH, mganga mkuu wa mkoa wa Geita Dokta Omary Sukari anasema Baiskeli hizo zitawasaidia kupunguza adha ya kutembea umbali mrefu kwa ajili ya kuwafikia waathirika wa maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
"Wateja wetu wote ambao wameanza huduma ya tiba na matunzo katika vituo vyetu wanapata tiba hiyo bila kukatishwa kwa njia moja au nyingine au kwa changamoto yeyote, sasa wito wangu kwa wenzetu ambao sasa wanakwenda kupewa hizi baiskeli ni kuhakikisha kwamba wanazitumia kwa malengo yaliyowekwa kwa maana ya kuwafikia wale wateja wetu ambao wanapata huduma katika vituo vyetu vya tiba na matunzo kwahiyo huo Ndio wito wangu kwao", alisema Sukari.
Meneja mradi wa MDH mkoa wa Geita dokta Nickolous Tarimo anasema moja ya lengo la kutoa msaada wa Baiskeli hizo kwa wahudumu wa ngazi ya jamii ili kuwapelekea Dawa majumbani na kujua maendeleo yao ya kiafya.
"Kwenye kutatua changamoto ya kuwafikia wateja wanaoishi na maambukizi popote pale walio ili wafikie katika kuwapelekea dawa either kuwakumbusha tarehe zao za Kliniki au kuwahudumia kuwapa ushauri nasaha, katika kufikia vituo 104 kwenye kutoa afua mbalimbali, za HIV, zikiwemo huduma za kujikinga, huduma za kuwapima na kuwajua wateja wapya wenye maambukizi na kuunganisha kwenye Kliniki za tiba na matunzo, kuwahudumia.
kuwachukua sampuli za virology na kuwapa huduma nyingine kama za ARV, dawa za kufubaza maambukizi", alisema Tarimo.
Kaimu katibu tawala mkoa wa Geita Deodatus Kayango amelitaka shirika hilo kuendelea kutoa huduma kuhakikisha wanapunguza maamukizi mapya kwenye mkoa wa geita.
"Imeonekana kwamba wanaohitaji huduma 80 elfu, muendelee kuwapa huduma ili ikiwesekana vile virusi vifubae kabisa mpaka afya zao zilendelee kuimarika na vile vile endeleeni kutoa Elimu kwa jamii ili kupunguza maambukizi hayo ikiwesekana hata mwaka ujao tuweze angalau kushuka hata kwa asilimia 4," alisema Kayango.