Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wahudumu wa Baa walalamikia udhalilishaji

Pic Mwandishi Wahudumu wa Baa walalamikia udhalilishaji

Mon, 19 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wahudumu wa vinywaji katika baadhi ya baa wilayani Nachingwea mkoani Lindi wamelalamika kufanyiwa vitendo vya unyanyasaji na baadhi ya wateja wanaojinasibu kuwa na nguvu ya dola huku wengine wakilalamika zaidi kunyanyaswa na wamiliki wa baa hizo kwa kuwakata fedha mara kwa mara jambo linalotajwa kuwadhorotesha na kuwanyima haki zao.

Wakizungumza katika kikao na Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, kikao kilichodhamiria kutazama mwenendo na changamoto katika upande huo wa viburudisho ambao unatajwa kukua kwa kasi na kuibadilisha wilaya hiyo, wahudumu wamelalamika kunyanyaswa na kufanyiwa ubabe na baadhi ya wateja wasumbufu huku kwa wingi wao wakionyeshwa kukerwa zaidi na vitendo vya matusi, kebehi pia kukatwa fedha na matajiri wao pale wawapo na udhuru.

Wakijibu hoja za manyanyaso na makato ya fedha kwa wahudumu, matajiri ambao ni wamiliki wa baa hizo na mameneja wamekiri kuwepo kwa shutuma za manyanyazo kwa wahudumu huku wakisema ya kwamba suala la makato ya fedha ni makubaliano baina yao na wahudumu wenyewe ndio kipaumbele chao hata wakiomba kazi na hutaka hivyo ili wawe huru.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live